Usajili BIG SIX

 


MSIMU wa  2019/20,  Liverpool ilitwaa ubingwa wa Premier kwa kukusanya pointi 99, ikiwa ni ubingwa wao wa kwanza wa michuano hiyo baada ya takribani miaka 30 kupita. Baada ya kutwaa
taji hilo, Liverpool ikaachana na Dejan Lovren na Adam Lallana na kuwaleta Thiago
Alcantara and Diogo Jota kuelekea msimu wa 2020/21. Chelsea wakavunja benki kwa kutoa pauni
220m kwa kumnunua Timo Werner, Kai Havertz. Manchester City wao wakanunua mabeki
wawili kwa pauni 100m, huku Arsenal wakasajili Thomas Partey kutoka Atletico Madrid.
Kila klabu ilipambana na kujijenga upya kwa ajili ya msimu wa 2020/21 ambao umemalizika hivi
karibuni. Pamoja na hayo yote, kila mmoja kwa msimu ambao umemalizika amevuna alichopanda.
Kilichobaki sasa ni kwamba, kuelekea msimu ujao wa 2021/22 wamejipanga vipi kuhakikisha
wanaimarisha vikosi vyao katika kuzidisha ushindani? Ndani ya Premier, kuna timu sita
maarufu ambapo baada ya kila moja kuona amefanya nini msimu uliomalizika, kuelekea msimu
mpya wanatakiwa kujiimarisha maeneo ambayo yameainishwa hapa. MAN UTD: BEKI WA
KATI Tangu mwaka 2016, Man United ilitumia pauni 150m kwa ajili ya mabeki Harry
Maguire, Victor Lindelof na Eric Bailly, lakini Kocha Ole Gunnar Solskjaer anaonekana
kutoridhika na machaguo ya mabeki hao. Sven Botman wa Lille ametajwa kuwaniwa na
Man United kutokana na kuonekana bora. Pia beki wa Juventus, Cristian Romero naye amekuwa
miongoni mwa mabeki wanaowindwa na United. Huyu thamani yake ni pauni 16m. LIVERPOOL: BEKI WA KATI Liverpool wana shida ya beki wa kati, baada ya msimu uliopita kuteseka kutokana
na kuwakosa Virgil van Dijk, Joe Gomez  na Joel Matip  waliosumbuliwa na majeraha. Timu hiyo tayari imemchukua Ibrahima Konate wa RB Leipzig. CHELSEA: STRAIKA Safu ya ushambuliaji ya Chelsea ikiwa na Timo Werner, Kai Havertz  na Hakim Ziyech, ilishindwa kutamba
huku kiungo Jorginho akiwa ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi
hichoa akifunga saba, wakati Werner, Mason Mount na Tammy Abraham
kila mmoja akifunga mabao sita. Kocha Thomas Tuchel anatakiwa



kusaka straika ili kuiimarisha zaidi  safu hiyo ambapo Erling Haaland wa
Dortmund anatajwa kuwaniwa na Chelsea. Thamani yake ni zaidi ya
pauni 100m. Kama Harry Kane ataondoka Tottenham na Chelsea wakawa
siriazi, huenda akatua ndani ya kikosi hicho. MAN CITY: STRAIKA
Ndiyo mabingwa wa Premier kwa msimu ambao umemalizika. Straika
wao mfumania nyavu, Sergio Aguero msimu ujao hatakuwa ndani ya
kikosi hicho, hivyo kwa sasa Kocha Pep Guardiola atatakiwa kusaka
mbadala wake. Man City wameweka mitego yao kwa Kane na Haaland, lakini
pia Robert Lewandowski ambaye alifanya kazi na Guardiola pale
Bayern Munich. TOTTENHAM: STRAIKA Baada ya Harry Kane kusema
anataka kuondoka ndani ya Tottenham, inabidi wajipange kusaka mbadala wake kwani
kuondoka kwake timu hiyo itabaki haina mfungaji matata.
Kama ataondoka, wanaotajwa kuchukua mikoba yake ni Tammy
Abraham, Danny Ings, Dominic Calvert-Lewin na Paulo Dybala.
ARSENAL: KIUNGO MSHAMBULIAJI  ani Ceballos na Martin
Odegaard wanatarajia kurejea Real Madrid baada ya
muda wa mkopo kumalizika, kwa maana hiyo Kocha Mikel Arteta
atakuwa na kazi ya kuziba nafasi zao. Arteta atakuwa
na kazi ya kusaka kiungo mshambuliaji bora wakati akiendelea kumkuza Emile Smith
Rowe ambaye  amekuwa akifanya vizuri ndani ya Arsenal, lakini kwa sasa timu hiyo
inahitaji fundi wa pasi katika eneo la kiungo kama ilivyokuwa kwa Mesut Ozil.
Imeripotiwa kuwa huenda Mjerumani, Julian Brandt akatua Arsenal, huku kipa Bernd
Leno akionekana kumshawishi. Thamani yake ni pauni 25m.

Previous Post Next Post

Translate