Kocha Simba ataja sababu za Kakolanya kusugua benchi

MILTON Nienov aliyekuwa kocha wa makipa ndani ya Simba ameweka wazi kuwa sababu kubwa iliyomfanya kipa
namba mbili wa timu hiyo, Beno
Kakolanya kushindwa kupata nafasi kikosi cha kwanza ndani ya Simba ni ugumu wa nafasi hiyo katika kufanya mabadiliko.

 

Raia huyo wa Brazil amebainisha kuwa kuna sehemu ambazo ni jambo rahisi kufanya mabadiliko ila eneo la kipa huwa linakuwa gumu kutokana na kumlinda yule anayeanza.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Nienov alisema kuwa katika kazi ya kuwapa nafasi makipa ni lazima kuzingatia utimamu wa mwili pamoja na utendaji wake kwenye kazi ambayo huwa anaifanya.

 

“Kuna makipa wazuri Simba ikiwa ni pamoja na Kakolanya, Kisubi (Jeremiah) lakini namba moja amekuwa akitumika mara kwa mara Manula huku Kakolanya akikaa benchi, na sababu ni ugumu wa nafasi katika kufanya
kazi.

 

“Ukiwa mwalimu kuna yule kipa namba moja na kuna chaguo la mwalimu na mara nyingi namba moja huwa anapenya kikosi cha kwanza jumla,” alisema Mbrazili huyo aliyechimbishwa ndani ya Simba Oktoba 26, kwa kile kilichoelezwa ni makubaliano ya pande zote mbili.


Wakati anasepa aliacha Simba
ikiwa imecheza mechi tano, Manula amecheza tano huku Kakolanya akiwa hajacheza hata moja.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

 

Previous Post Next Post

Translate