REKODI ya kipa namba moja wa Simba kuweza kucheza mechi
nyingi bila kufungwa imetibuliwa na nyota wa Ruvu Shooting, Elias Maguli
baada ya kumtungua walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba wakati ubao
uliposoma Ruvu Shooting 1-3 Simba.
Manula alikuwa ni namba moja kwa makipa ambao hawajafungwa kwenye
mechi nyingi za Ligi Kuu Bara ambapo alikuwa amecheza jumla ya mechi
tano ambazo ni dakika 450 bila kufungwa rekodi ambayo ilikuwa ni bora
kwake.
Mshindani wake mkubwa alikuwa ni Diarra Djigui wa Yanga ambaye kwa
sasa ana clean sheet nne kwenye mechi sita kwa kuwa alifungwa pia kwenye
mchezo dhidi ya Namungo FC wakati ubao wa Uwanja wa Ilulu Lindi
uliosoma Namungo 1-1 Yanga na bao lake la kwanza kufungwa Bongo kwenye
ligi ilikuwa mbele ya Ruu Shooting ambapo ni Shaban Msala alimuachia
msala.
Manula anapambana kuweza kutetea tuzo ya kipa bora kwa kuwa
aliitwaa tuzo hiyo msimu wa 2020/21 baada ya kufanya vizuri na kukusanya
clean sheet 18 hivyo ana kazi kubwa ya kuweza kutetea tuzo hiyo.
Tayari amecheza mechi sita na amekusanya clean sheet tano kwenye
mechi alizocheza huku akiwa bado ni namba moja kwa makipa ambao
wamefungwa mabao machache kwenye mechi sita ndani ya ligi.
Dakika zake 90 mbele ya Kocha Mkuu, Pablo Franco alikwama kuweza
kuokoa mchomo uliopigwa ndani ya 18 na Maguli jambo ambalo limetibua
rekodi yake mapema kwa kuwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes na hata
mikoba ilipokuwa mikononi mwa Hitimana Thiery pamoja na Seleman Matola
hakuweza kufungwa.
Kikosi cha Simba kwenye msimamo kipo nafasi ya pili kimekusanya
pointi 14 huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi 16 baada ya kucheza
mechi sita.
Tags
soka