AZAM FC YAITULIZA MTIBWA SUGAR JUMLAJUMLA

 

AZAM FC usiku wa kuamkia leo Desemba Mosi wameitungua Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ushindi kwa Azam FC unaipa mwendo mgumu Mtibwa Sugar kwa kuwa haijui ladha ya ushindi mpaka sasa baada ya kucheza mechi saba na kibindoni ina pointi zake mbili.

Ni bao la Idrisa Mbombo ambaye alipachika bao hilo dakika ya 51 baada ya mabeki wa Mtibwa Sugar kufanya makosa ya kumuacha peke yake akimalizia pasi ya Bruce Kangwa.

Haikuwa furaha kwa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ambaye alipoteza furaha kutokana na kichapo hicho.

Sasa Azam FC inafikisha pointi 10 ikiwa nafasi ya sita huku Mtibwa Sugar ikibaki na pointi zake mbili nafasi ya 16.

Previous Post Next Post

Translate