CHEKA,ALKASUSU WAPIMA UZITO,LEO VITASA VINAPIGWA

 

Cheka, Alkasusu wapima uzito, kupasuana leo

MABONDIA Cosmas Cheka na Muhsini Swalehe ‘Alkasusu’ wamepima uzito jana tayari kwa pambano la ubingwa wa taifa wa TPBRC litakalopigwa leo kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar.

Mabondia wamepima uzito katika pambano hilo ambalo limeandaliwa na kampuni ya Grobox Sports Promotion lililopewa jina la Usiku wa Mishindo ambapo kiingilio cha pambano hilo ni Sh 20,000 kwa VIP ma Sh 7,000 kawaida.

Wengine waliopima uzito ambao watacheza mapambano ya utangulizi ni Albano Clement na Ramadhan Mbegu, Pius Mpenda na Ambokile Chusa, Kheri Rashid na Hamadi Furahisha.

Shaban Abdallah yeye atacheza na Alois Kabinda wakati Oscare Richard atapanda ulingoni kumalizana na Charles Malele.

Hivi karibuni Cheka ameingia kwenye mzozo na mashabiki wa mchezo huo kutokana na tabia yake ya kukimbia mechi kwa kisingizio cha kuumia mkono kama alivyofanya katika pambano lake na Issa Nampepeche kwa kudai kuwa alikuwa amepata ajali iliopelekea kuvunjika mkono.

Previous Post Next Post

Translate