LIVERPOOL ETI BILA ORIGI HAKUNA MPIRA

 

BAADA ya kupachika bao la ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu England dakika za lala salama, Divock Origi, mabosi wa timu hiyo wameweka wazi kuwa mpira bila nyota huyo bado haujakamilika.

Orogi alipachika bao hilo dakika ya 90+4 mbele ya Wolves akitumia pasi ya mshambuliaji Mohamed Salah raia wa Misri akiwa ndani ya 18 kwa utulivu mkubwa kwa kuwa mabeki wa timu pinzani walikuwa ni imara mwanzo mwisho.

Ilikuwa ni Uwanja wa Molineux maajabu hayo yalitokea kwa kuwa Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp alikuwa akiamini huenda wangepata pointi moja pekee wakiwa ugenini.

Nyota huyo ambaye alitoka benchi alipachika bao la ushindi na kuifanya Liverpool kusepa na pointi tatu mazima na kufanya wafikishe jumla ya pointi 34 nafasi ya pili huku Wolves ikibakiwa na pointi 21 nafasi ya 8.

Rekodi zinaonyesha kuwa Origi ni mzuri akianzia benchi kwa kuwa amekuwa akifunga mabao muhimu katika kutimiza majukumu yake na Klopp amesema kuwa mchezaji huyo ni Legend.

“Origi ni Legend anafanya mambo mazuri kwa ajili ya timu,”.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Liverpool waliachia bao la nyota huyo na kuweka ujumbe wa kumsifu mchezaji huyo huku wakieleza kuwa mpira bila Origi unakuwa bado haujawa mpira.

Previous Post Next Post

Translate