NASREDDINE
Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kwamba hakuna mchezaji mkubwa
ndani ya kikosi cha Yanga kwa kuwa Yanga ni kubwa kuliko yoyote.
Kocha huyo
raia wa Tunissia ameongeza kuwa kuhusu kuanza kikosi cha kwanza kwa
wachezaji wake itategemea na namna hali itakavyokuwa kutokana na mchezo
husika na haina maana kwamba kufunga mabao ni sababu ya kuweza kuanza
kikosi cha kwanza.
Ikumbukwe
kwamba nyota wake Heritier Makambo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho
dhidi ya Ihefu FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa aliweza kufunga mabao
matatu lakini Nabi amebainisha kwamba hawezi kuwa na uhakika wa kuanza
kikosi cha kwanza.
“Kila
mchezaji ndani ya Yanga ni muhimu na ipo wazi kwamba Yanga ni kubwa
kuliko mchezaji hivyo haina maana kwamba kufunga ama kutofunga ni sababu
za mchezaji kuanza kikosi cha kwanza.
“Ninafurahishwa
na uwezo wa wachezaji wangu wote kila mmoja anatimiza majukumu yake
kuhusu kuanza ama kutokuanza kikosi cha kwanza wote wanastahili kucheza
na inategemea na mbinu ya mchezo husika,”amesema.