BARBARA:WACHEZAJI WANAOMBA KUCHEZA SIMBA

 

WACHEZAJI wanaomba kucheza Simba

MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa wachezaji wengi wanaomba kucheza ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Kwa sasa Simba ni timu pekee ambayo inakibarua cha kupeperusha bendera kimataifa ikiwa inashiriki Kombe la Shirikisho baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo wake wa kwanza katika Kombe la Shirikisho hatua ya mtoano ilifanikiwa kushinda mabao 3-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia ina kibarua cha kwenda kusaka ushindi kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Desemba 5.

Barbara amesema kuwa amekuwa akiwasiliana na mawakala wengi wa wachezaji wakiomba wachezaji wao waweze kusajiliwa katika timu hiyo.

“Nimekuwa nikiwasiliana na mawakala wengi ambao wanapenda kuona wachezaji wao wakicheza ndani ya Simba,” amesema.

Previous Post Next Post

Translate