BOSI MPYA MANCHESTER UNITED KUANZA NA ARSENAL

 

KLABU ya Manchester United imemtangaza Ralf Rangnick kuwa kocha wa muda wa kikosi hicho mpaka mwishoni mwa msimu huu wa 2021/22 akichukua nafsi ya kocha Ole Gunnar Solskjaer aliyefutwa kazi wiki iliyopita.

Rangnick atasalia Manchester United pindi mkataba wake wa miezi 6 kama kocha wa muda utakapo salia lakini atakuwa na jukumu la kuwa mshauri wa mambo ya kiufundi kwa mkataba wa miaka miwili (2). Lakimi imaripotiwa anaweza akasalia kama kocha mkuu endapo kama matokeo yatakuwa mazuri.

Baada ya kutambulishwa rasmi kocha huyu mwenye heshima kubwa nchini Ujerumani kutokana na mtindo wake wa kufundisha soka la kushambulia zaidi amesema:-“Ninafuraha kujiunga na Manchester United na malengo ni kuufanya msimu huu kuwa wa mafanikio kwa klabu. Kikosi kina wachezaji wenye vipaji na kina uwiano mkubwa wa vijana na wenye uzoefu.

“Juhudi zangu zote kwa miezi sita ijayo zitakuwa kusaidia wachezaji hawa kufikia ubora wao, kwa mchezaji mmoja mmoja na muhimu zaidi timu kwa ujumla. Zaidi ya hayo ninatarajia kuunga mkono malengo ya muda mrefu ya klabu kwa misingi ya ushauri.” Amesema Rangnick.

Mchezo wa Ligi Kuu wa Manchester United unaofata dhidi ya Arsenal wa Desemba 2, 2021 unaweza kuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Rangnick kukiongoza kikosi hicho akiwa kama kocha mkuu, lakini kama vibali vyake vya kufanya kazi vitakuwa vimekamilika.

Previous Post Next Post

Translate