MAYELE HATARI YAKE NI KILA BAADA YA DAKIKA 399

 

 

MSHAMBULIAJI Fiston Mayele raia wa DR Congo mali ya Yanga ambao ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi sita na kufunga jumla ya mabao 10 amehusika kwenye mabao matatu .

Nyota huyo ambaye ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi amefunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao ambalo lilifungwa na Feisal Salum.

Kwenye mechi sita ambazo amecheza nyota huyo ametumia jumla ya dakika 402 akiwa na wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 399.

Mchezo wake wa kwanza ilikuwa mbele ya Kagera Sugar hapa alitumia dk 88,ilikuwa Uwanja wa Kaitaba mchezo wa pili ilikuwa mbele ya Geita Gold,hapa alitumia dk 64,ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Mbele ya KMC wakati akitumia dk 78,Uwanja wa Majimaji hapa alifunga bao lake la kwanza na kutoa pasi yake ya kwanza pia na mchezo wan ne ilikuwa dhidi ya  Azam FC alitumia dk 90 na alifunga bao lake la pili ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Walipokutana na Ruvu Shooting alitumia  dk 90,Uwanja wa Mkapa na kwenye mchezo wake huu wa tano anakumbuka alipiga jumla ya mashuti saba yaliyolenga lango ila yaliokolewa na kipa Mohamed Makaka wa Ruvu Shooting.

Kete yake ya sita ilikuwa mbele ya Namungo,alitumia dk 82, Uwanja wa Ilulu. Mabao yake yote mawili amefunga kwa kutumia mguu wa kulia na pasi yake ametoa kwa mguu wa kushoto.

Previous Post Next Post

Translate