HERRY SASII KAONYESHA INAWEZEKANA LICHA YA MAKOSA MADOGO

 

KIVUMBI kinazidi kuwaka kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo kwa msimu huu mpya wa 2021/22 unaoyesha kwamba sio wa kitoto.

Wakati ligi inazidi kupamba moto waamuzi wamekuwa ni wimbo unaoimbwa kila wakati kutokana na maamuzi yao kuwa ya maumivu kwa upande mmoja.

Makosa yapo lakini haina maana kwamba yawe yanajirudia mara kwa mara hii naona kwamba haipo sawa nina amini kwamba waamuzi wana uwezo mkubwa na wanaweza kufanya kazi kwa umakini tena wa hali ya juu.

Kwa upande wa matokeo ambayo yanapatikana ni suala la wale wachezaji ambao wameweza kusajiliwa pamoja na kuongezewa mikataba kwenye timu zao ambazo wapo kwa wakati huu.

Tumeona kwenye mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa shauku kubwa kati ya Simba na Yanga namna mwamuzi wa kati Herry Sasii alivyoweza kutimiza majukumu yake.

Katika hilo pongezi anastahili namna ambavyo aliweza kuhimili ile presha na kuwa rafiki wa wachezaji na kuwaonya pale inapostahili.

Kwa ambayo yanatokea basi nina amini kwamba kuna kitu cha kujifunza na inamaanisha kwamba inawezekana waamuzi wakafanya vizuri.

Matokeo ambayo yanatokea uwanjani kila baada ya mechi kwa waamuzi kulalamikiwa hii sio sawa pongezi kwa jopo zima la waamuzi kwa kutimiza majukumu yenu kwa umakini.

Ikumbukwe kwamba timu zinatumia dakika 90 kuweza kupata maamuzi ya kile ambacho walikifanya yule atakayetumia makosa ya mpinzani wake huonekana ni mshindi na hicho ndicho ambacho mashabiki wanahitaji.

Ikiwa ni mpango ambao unachorwa na watu walio kwenye ulimwengu wa michezo wanapaswa kuacha tabia hiyo.

Tukiachana na timu, mchezaji kwa sasa ana kazi ya kutimiza majukumu yake kwa usahihi ndani ya uwanja ili kurejesha imani kwa mashabiki ambao wanawaamini.

Kwa kuwa maisha ya soka lazima yaendelee mchezaji mmoja kuondoka na kwenda katika timu nyingine hilo halizuiliwi.

Kwa kuwa tayari ligi imeshaanza basi ni muhimu kuona kwamba kila mmoja anapaswa kutimiza majukumu yake ipasavyo hii itafanya ushindani kuwa imara na bora.

Rai yangu kubwa hasa kwa waamuzi ambao ni sehemu ya mchezo na mafanikio ya mpira wetu wanapaswa wasipepese macho katika kazi yao ndani ya uwanja.

Ipo wazi kwamba, waamuzi ni binadamu na makosa yapo lakini haipaswi iwe kila siku wao wanabebeshwa zigo la lawama kila baada ya mchezo kuiisha hii haifai.

Kusimamia kwao majukumu ambayo wamepewa kwa uzuri kutaongeza ule ushindani kufanya kila timu kupata ushindi baada ya dakika 90 bila kuwa na sehemu ya kushusha lawama.

Kila timu kwa sasa inahitaji pointi tatu muhimu hilo lipo wazi na kwa namna mambo yanavyokwenda hivi ndivyo inatakiwa kuwa mpaka mwisho wa msimu.

Malalamiko yamekuwa mengi lakini yanaweza kupungua ikiwa tu waamuzi  watasimamia sheria 17 na kufanya maamuzi sahihi ni tiba tosha kwa haya malalamiko ambayo yamekuwa yakiskika kutoka kwa viongozi.

Sasii ameonyesha kitu licha ya kwamba kuna mapungufu ambayo ameonyesha ikiwa ni pamoja na kusimamisha mpira wakati timu ikiwa kwenye mashambulizi.

Hamna namna wakati mwingine ni lazima haya yafanyiwe kazi ili kuweza kuboresha zaidi kwenye sekta ya maamuzi.

Previous Post Next Post

Translate