KLOPP ANAAMINI KWAMBA GERRARD ATAKUWA KOCHA MPYA LIVERPOOL

 

Soccer Football - Premier League - Aston Villa v Leicester City - Villa Park, Birmingham, Britain - December 5, 2021 Aston Villa manager Steven Gerrard and Ashley Young celebrate after the match Action Images via Reuters/Jason Cairnduff EDITORIAL USE ONLY. No use with unauthorized audio, video, data, fixture lists, club/league logos or 'live' services. Online in-match use limited to 75 images, no video emulation. No use in betting, games or single club /league/player publications. Please contact your account representative for further details.

KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp anaamini kwamba Steven Gerrard yupo kwenye njia bora zaidi ya kuwa kocha mpya ndani ya kikosi hicho siku za usoni.

Gerrard kwa sasa ni kocha wa Aston Villa na wikiendi alikuwa ndani ya Uwanja wa Anfield akiwa na timu ya Aston Villa ambapo walikuwa na mchezo wa Ligi Kuu England.

Katika mchezo huo Liverpool iliweza kushinda bao 1-0 na kusepa na pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Klopp ameweka wazi kwamba kocha huyo mwenye miaka 41 hakuna jambo ambalo linaweza kumzuia kuwa hapo ndani ya Liverpool kwa miaka kadhaa ijayo.

Alipoulizwa kama anaweza kumuachia kiti Gerrard ambaye aliwahi kuwa nahodha wa Liverpool zamani alisema kwa kujiamini:”Ndiyo, nafikiri ni mtu sahihi kabisa.

“Tatizo ni kama sasa ni muda sahihi kwake, tulimuona Frank, (Lampard) akiwa na Chelsea. Alifanya kazi nzuri sana lakini ni kocha mchanga sana kwenye nafasi ile.

“Mimi siyo ambaye natakiwa kuchagua kocha hapa, sijui nini unatakiwa kufanya ili uwe kocha wa Liverpool.”.

Previous Post Next Post

Translate