SIMBA YAIVUTIA KASI YANGA ZAMBIA

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuwakutanisha mabingwa watetezi  Simba pamoja na Yanga, Desemba 11, mbinu za Pablo Franco zimeanza kutumika nchini Zambia.

Simba ilikuwa huko kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Jumapili ya Desemba 5 na baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Heroes ulisoma Red Arrows 2-1 Simba.

Lakini Simba iliweza kusonga mbele katika hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 wa kuwa kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa Simba ilishinda mabao 3-0.

Kikosi hicho hakijarejea Dar na badala yake kimebaki Zambia kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa watani wa jadi ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mpaka sasa timu hizo mbili kwenye mechi saba ambazo wamecheza hakuna ambayo imepoteza mchezo zaidi ya kuambulia sare pekee.

Yanga ni vinara wakiwa na pointi 19 wanafuatiwa na Simba walio nafasi ya pili na pointi 17 kibindoni.

Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo na Simba imelazimisha sare kwenye mechi mbili ilikuwa dhidi ya Biashara United 0-0 na Coastal Union pia ilikuwa 0-0.

Previous Post Next Post

Translate