WAPINZANI WA SIMBA WAPANIA KULIPA KISASI ZAMBIA

 

UONGOZI wa timu ya Red Arrows ya Zambia, umeweka wazi kuwa umepanga kulipa kisasi katika mchezo
wa marudiano dhidi ya Simba 
licha ya kufungwa mabao mengi kutokana na mvua iliyoharibu hali ya uwanja na kukwamisha mipango yao.

Timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Anga la Zambia, imepoteza mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho kwa mabao 3-0 dhidi ya Simba kabla ya mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa Jumapili ya Desemba 5 huko Zambia ambapo mshindi wa jumla ataenda makundi Shirikisho

 Meneja wa timu hiyo Rio Flowers, amesema: “Tunaamini sasa ni wakati wa kulipiza kisasi cha kuhakikisha tunawaondoa kwa kuwafunga mabao mengi ili kuzidi yale ambayo wao wametufunga huko.

“Ukweli tunawaheshimu kwa sababu ni timu bora lakini kwa upande wetu tunachotaka kukifanya ni kuhakikisha tunapata ushindi mkubwa hapa kwetu.”

Leo kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kinatarajiwa kuibuka nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa kimataifa.

Previous Post Next Post

Translate