YANGA YAANZA MAZUNGUMZO NA CHAMA

 

UONGOZI wa Yanga umeanza rasmi mazungumzo na wakala wa kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chama
anayekipiga Klabu ya 
RS Berkane ya nchini Morocco.


Hiyo ikiwa ni siku chache 
tangu uongozi wa Yanga kuanza mazungumzo na Berkane inayommiliki baada ya kumnunua kutoka Simba kwa dau la Sh 1Bil.

Mzambia huyo alijiunga na Berkane katika msimu huu  baada ya timu hiyo kufikia muafaka mzuri na Simba kwa ajili ya kumnunua.


Mmoja wa mabosi 
wa Yanga, amesema kuwa, wapo katika hatua za mwishoni za kukamilisha usajili wa kiungo huyo baada ya kupeleka ofa nzuri Berkane.


Bosi huyo 
amesema kuwa Yanga wanapata ujasiri wa kumpata kiungo huyo kutokana na ukaribu na maelewano
mazuri na 
wakala huyo aliyefanikisha usajili wa Yannick Bangala na Shaban Djuma.

Aliongeza kuwa wakala huyo hivi karibuni alitembelea katika kambi ya Yanga huko Avic Town, Kigamboni kwa ajili
ya kufuatilia 
mazoezi ya timu hiyo wakijiandaa na mchezo wa Ligi
Kuu Bara.


“Yanga 
wana asilimia kubwa ya kumsajili Chama, licha ya klabu yake ya zamani ya Simba kupewa nafasi kutokana na mkataba wake kumbana.


“Mkataba wa 
Chama wa kutoka Simba kwenda Berkane ni mgumu, hivyo ili asaini Yanga ni lazima wauvunje mkataba wake ambao wenyewe wapo tayari kutoa kitita chochote cha pesa ili kukamilisha dili hilo.


“Simba wenyewe 
wanaonekana kushindwana naye kutokana na dau kubwa la Sh 1Bil ambalo wanalihitaji
Berkane ili wamuachie kiungo 
huyo ambaye inaelezwa hafurahii maisha ya Morocco,” alisema bosi huyo.


Alipotafutwa Makamu 
Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema:
“Tupo kwenye mazungumzo 
na wachezaji wengi kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo, hivyo huenda Chama akawepo au asiwepo katika mipango yetu.”

Previous Post Next Post

Translate