Curry Aweka Rekodi NBA

 

STAA wa Golden State Warriors, Stephen Curry, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza mwenye 3-pointi nyingi ndani ya NBA.

 

Curry aliweka rekodi hiyo hivi karibuni akifikisha 2,974 katika robo ya kwanza ya mchezo wa NBA dhidi ya New York Knicks kwenye Dimba la Madison Square Garden akifanya mashambulizi matatu tu.

 

Staa huyo amevunja rekodi ya Ray Allen, ambaye alikuwa nayo tangu 2011 akiwa anaitumikia Boston Celtics.

 

Baada ya kuweka rekodi hiyo, mchezo ulisimamishwa, ambapo Curry alikwenda kukumbatiana na wachezaji wenzake. Katika mchezo huo, alikuwepo Allen na baba yake ambao walimpongeza.

Previous Post Next Post

Translate